Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara
ikitarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 12, mwaka huu, Kocha wa Mwadui FC,
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ndiye kocha pekee ambaye amefanikiwa kujipima na nusu
ya timu zote za ligi hiyo.
Ligi hiyo itashirikisha timu 16 huku
yeye akijipima na timu tisa ambazo zinatarajiwa kushiriki ligi hiyo huku Mwadui
ikiwa imepanda na utakuwa msimu wake wa kwanza ingawa miaka takribani 20
iliyopita iliwahi kucheza ligi hiyo.
Kabla ya ligi kuanza Jumamosi ijayo,
kikosi cha Mwadui katika maandalizi yake kimecheza mechi na timu za madaraja
mbalimbali kuhakikisha tu kinajiweka fiti kwa ajili ya msimu mpya.
Julio, katika kuhakikisha mambo
yanakwenda sawa, alicheza na timu tisa za ligi kuu, ikiwemo Kagera Sugar, Stand
United na Toto Africans. Hizi alikutana nazo katika michuano ya Ligi ya Kanda
ya Ziwa ambapo waliibuka mabingwa.
Timu nyingine ambazo alicheza nazo ni
pamoja na Simba (Taifa), Africans Sports na Coastal Union (Mkwakwani), Azam FC
(Azam Complex) na JKT Ruvu (Karume).
Kocha huyo
alifunguka hivi: “Mimi kama kocha nilikuwa na programu zangu kuhakikisha
najenga timu yenye ushindani, nimecheza michezo mingi na timu tofauti na
wachezaji wangu wamejifunza mengi bila kujali ni timu gani walikutana nayo,
zaidi tutakutana kwenye ligi,” alisema Julio.
0 COMMENTS:
Post a Comment