Kocha wa timu ya taifa ya Libya, Javier Clemente amesema alijua Tanzania itaipa Nigeria wakati mgumu.
Akizungumza kutoka Madrid Hispania, Clemente ambaye ni kocha wa zamani wa Atletico Madrid, Athletico Bilbao na Vilarreal amesema, Tanzania ilikuwa na kila sababu ya kufanya vizuri zaidi.
"Nimesikia matokeo ni sare ya bila mabao, mwambie kocha na timu yake nzima ya ufundi hongera sana. Timu yake ni yenye vijana wengi na ina nafasi.
"Kilichofanya niamini Tanzania itaipa wakati mgumu Nigeria ni kasi, jambo ambalo lingeisumbua Nigeria ambayo ina soka la taratibu.
"Nimefuatilia na kuona kundi lenu mko pia na Misri, si kazi lahisi lakini kujiamini ni jambo jema sana," alisema.
Stars ilicheza mechi ya kirafiki ya mazoezi dhidi ya Libya wakati ikiwa kambini nchini Uturuki na kufungwa kwa bao 2-1.
Mechi hiyo ilianza na mzozo baada ya Libya kuipitisha kama mechi ya kirafiki inayotambulika na Fifa na Caf, jambo ambalo TFF kupitia mkuu wa msafara, Msafiri Mgoyi walilikataa katakata.
Lakini baada ya makubaliano, soka safi na la kuvutia likachezwa na hata baada ya mechi, Clemente akatoa sifa zake kwa Stars kwa ilicheza na kuwabana sana hasa katika kipindi cha pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment