Kesi inayomkabili kipa wa Mbeya City,
Juma Kaseja dhidi ya klabu ya Yanga imeahirishwa hadi mwishoni mwa mwezi ujao.
Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama
ya Kazi Kitengo cha Usuluhishi imeshindwa kusikilizwa baada ya kutokuwa na
umeme.
Yanga inamshitaki Kaseja kwa madai ya
kukiuka mkataba wake, kushindwa kwenda kazini bila ya taarifa jambo ambalo
lilikuwa ni kinyume na makubaliano yao.
Kutokana na tatizo hilo ambalo sasa
ni nchi nzima baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo limekuwa
halina uhakika na mambo mengi kutangaza linafanya marekebisho kupitia mtambo wa
Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Tanesco imetangaza siku moja tu kabla
ya kukata umeme, jambo ambalo limeleta usumbufu mkubwa kwa wakazi na wateja
wake.
Kutokana na hali hiyo, kazi sehemu
mbalimbali zikiwemo katika ofisini za serikali na binafsi zimesimama kabisa
ingawa bado wachumi hawajaeleza kwamba taifa litaingiza kiasi gani kutokana na
hatua hiyo.
Sasa kesi ya hiyo ambayo Yanga ni
mlalamikaji na Kaseja ni mshitakiwa itasikilizwa mwezi ujao mwishoni, matarajio
yakiwa Tanesco watakuwa wamerudisha umeme mambo yaende kama yanayotakiwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment