DULE (WA PILI KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA MWINYI KAZIMOTO. KULIA NI DYLAN KERR NA SELEMANI MATOLA. |
Kocha wa viungo wa Simba, Mserbia Dusan
Momcilovic ‘Dule’, amesema ameshamaliza kazi ya kuwafanya wachezaji wake wawe
fiti kupambana dakika 90 uwanjani kilichobaki ni utekelezaji tu.
Dule aliyeletwa na uongozi wa timu hiyo
kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti, amefanya kazi na timu hiyo kwa muda
usiopungua miezi miwili hadi sasa na amesisitiza kuwa vijana wake wameiva.
Kazi ya kocha huyo ilianzia Lushoto mkoani
Tanga ambako Simba iliweka kambi kwa wiki mbili, kisha wakaenda Zanzibar halafu
wakarejea Dar es Salaam kabla ya kurudi Zanzibar kujiandaa na msimu ujao wa
Ligi Kuu Bara.
Dule, alisema kuna mabadiliko makubwa kwa
wachezaji wake tangu alipowasili nchini na sasa na wapo vizuri katika nguvu na
pumzi.
“Sasa wachezaji wapo sawa kwa fiziki uwanjani,
wakiwa mazoezini wanafanya vizuri bado vile vitu wanatakiwa kuvionyesha kwenye
mechi, kazi kwao,” alisema Dule.
0 COMMENTS:
Post a Comment