September 5, 2015


Uongozi wa Yanga umetinga katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuomba vibali vya wachezaji wake wanane ili waweze kupata uhalali wa kuichezea timu yao katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Yanga imesajili wachezaji wapya saba ambao ni Donald Ngoma, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke, Malimu Busungu, Geoffrey  Mwashiuya, Mudathir Khamis na Simon Matheo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema wamepeleka barua TFF kuomba vibali vya wachezaji hao pamoja na ‘ku-renew’ vile vya wachezaji waliokuwepo kikosini tangu awali.

“Tumepeleka barua TFF ya kuomba vibali vya wachezaji wetu wanane baada ya kukamilisha zoezi la usajili msimu huu kwa mujibu wa taratibu, mambo yakienda vizuri tutawatumia msimu huu,” alisema Tiboroha.

Straika Ngoma ni miongoni mwa nyota wa Yanga wanaotarajiwa kufanya vizuri katika kikosi cha timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ikiwemo ile ya watani dhidi ya Simba, Septemba 26, mwaka huu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic