September 20, 2015




MPIRA UMEKWISHAAA
Dk 90+3
GOOOOOOO Kiiza tena, DK 90 anafunga bao safi baada ya kupokea basi safi ya Kazimoto

Dk 89 Kazimoto anaumia na kutolewa nje kwa matibabu, Simba wanacheza pungufu
Dk 83&87 timu zinashambuliana kwa zamu, Kagera Sugar wanafanya mashambulizi mawili, hali kadhalika Simba lakini umakini

SUB: DK 81, Simba wanamtoa Ajibu na anafasi yake inachukuliwa na Mwinyi Kazimoto

Dk 80, Masumbuko anamtoka Isihaka na kupiga krosi safi lakini Kessy anafanya kazi ya ziada kuokoa
SUB: Dk 77 Anaingia Abuu Mtiro Mtiro kuchukua nafasi ya Said Isihaka

Dk 75, N'daw akiwa katika nafasi nzuri lakini anapiga kichwa mtoto kabisa

Dk 64 hadi 67, Kagera wanaonekana kubadilika na kushambulia mfululizo lakini wanapoteza nafasi nyingi
SUB Dk 61 Simba inamtoa Nimubona anaingia Kessy, inamtoa Sserunkuma anaingia Nd'aw

Dk 58, Simba wanaendeleza mashambulizi, Ajibu anapiga krosi saaafi lakini Kiiza anashindwa kufunga
Dk 56, Simba wanafanya shambulizi jingine, krosi safi ya Kanoni inamfikia Kiiza, anapiga lakini Kanoni anaokoa

Dk 54, pasi nzuri ya Mwalyanzi, Ajibu anajaribu lakini kipa Kagera anaokoa na kuwa kona, lakini haina manufaa

GOOOOO Dk 50, Mbarak Yusuf anafunga bao safi baada ya kumchambua Hassan Isihaka 

SUBDk 49 Kagera wanamtoa Iddi Kulachi nje, anaingia Kenneth MAsumbuko
Dk 48 Ngwai anajaribu shuti kali lakini anasshindwa kulenga
GOOOOOO Dk 46, mpira safi Tshabalala, unamkuta Kiiza anapachika bao saaafi kwa kichwa na kuiandikia Simba bao la pili

MAPUMZIKO
Dk 45+5
KADI 45 Simon Sserunkuma analambwa kadi ya njano kutokana na kucheza rafu kwa makusudi kabisa

DK Dk 44, Shambulizi kali kwenye lango la Simba, mpira mzuri wa Kavila lakini Manyika anaudaka, unamtoka lakini anauwahi

KADI DK 41, Babu Ally analambwa kadi ya njano kwa kumkanyaga Mwalyanzi kwa makusudi kabisa

DK 37, Kona safi ya Ajibu, Kiiza anapiga kichwa safi lakini anashindwa kulenga
Dk 32, Ajibu anaingia vizuri lakini Kanoni anaokoa vizuri na kona ambayo haina matunda

GOOOOOOO Dk 30, Kiiza anaifungia Simba bao safi kwa kichwa akiunganisha krosi safi kutoka magharibu mwa uwanja

SUB Dk 29, Kagera wanamtoa Lawrance Mugia anaingia Babu Ally
Dk 29, Paul Ngwai anaingia vizuri na kupiga shuti kali lakini linaishia mikononi mwa Manyika

Dk 21, Awadhi Juma anapata pasi nzuri ya Ndemla, katika nafasi nzuri anampa kipa mikononi

Dk 19, Simba wanafanya shambulizi kali lakini Kiiza anashindwa kufunga na mabeki wanaokoa na kuwa kona.

Dk 12 hadi 15, Mpira unaonekana kuchezwa katikati ya uwanja zaidi huku kila timu ikionekana kuvizia
Dk 9, krosi saafi ya Emiry Nimubona inaingia kwenye lango la Kagera lakini Kiiza anachelewa

Dk 5, Issi Kulachi anamjaribu kipa Peter Manyika kwa shuti kali lakini analikamata kwa ulaini
Dk 3, Ajibu anatengeneza nafasi na kupiga shuti kali, hata hivyo anapaisha juuuu

Dk 2 Simba wanaanza kwa kufanya shambulizi, Mwalyanzi anaingia vizuri lakini anachelewa na mabeki wa Kagera wanaokoa.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic