Hamisi Kiiza ukipenda muite Diegeo,
ameifungia Simba mabao matatu na kuizamisha Kagera Sugar kwa 3-0.
Kiiza amefunga hat trick hiyo leo
wakati Simba ikicheza mechi yake ya tatu ya Ligi Kuu Bara.
Kwa ushindi huo unamuwezesha Kiiza
aliyewahi kuichezea Yanga kufikisha mabao matano katika mechi tatu.
Simba ilicheza vizuri katika kipindi
cha kwanza na kufanikiwa kupata bao moja lililodumu hadi mapumziko.
Bao la pili la Kiiza lilifuatia
katika dakika ya 46 kabla ya Kiiza tena kufunga jingine katika dakika ya 90.
Simba itashuka dimbani tena Jumamosi ijayo kuwavaa Yanga, mechi inayotarajiwa kuwa ya kukata na mundu.
0 COMMENTS:
Post a Comment