September 19, 2015



MPIRA UMEKWISHAAAAA

DK 90+ 3GOOOOOOO Dk 87 anapiga shuti saaafi la chini na kuandika bao la nne kwa Yanga
SUB Dk 82 Anaingia Busungu kuchukua nafasi ya Ngoma

 Dk 81, JKT wanapata kona, krosi nzuri ya Juma lakini Barthez anajaribu kuokoa na kugongana na Mwaikimba. Mwamuzi anasema faulo

Dk 80, nafasi nyingine ya Msuva , lakini shuti lake linapita juu ya lango la JKT
Dk 76, Msuva anaingia vizuri kwa mara nyingine, anapiga shuti kali lakini mpira unapiga nyavu za nje, goal kick

Dk 69 Msuva anapiga shuti kali kabisa huku akimlaghai kipa kama anataka kutoa krosi lakini anaokoa na kuwa kona ambayo mwisho haina matunda

SUB Dk 67, JKT inamtoa Saad Kipanga anaingia Emmanuel Pius

GOOOOOOOO Dk 62 Tambwe anaifungia Yanga vao safi kabisa la kichwa baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Twite

SUB Dk 61 Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya

 DK 58, Yanga wanafanya shambulizi kali sana, lakini Tambwe anashindwa kuuufikia mpira wa krosi wa Msuva, mabeki JKT wanaondosha hatari

SUB Dk 57 anaingia Mwaikimba kuchukua nafasi ya Kamuntu
Dk 56, Twite anapiga shuti kali sana linapita hatua chache kidogo ya lango la Priosns

GOOOOOOO Dk 50 Aidan anageuka vizuri na kufnga bao saafi ambalo ni bao la kwanza Yanga kufungwa msimu huu leo ikiwa inacheza mechi ya tatu

 DK 49 JKT wanafanya shambulizi kali na kufanikiwa kupata faulo ambayo Michael Aidan anashindwa kufunga.
GOOOOOOOOO Dk 48, Tambwe anafunga bao zuri baada ya kipa wa JKT kuutema mpira wa krosi wa Kaseke, Tambwe akauwahi na kuutumbukiza kimyani kwa ulaini kabisa.

Dk 46, Juma anaingia na mpira vizuri, anafanikiwa kumtoka Haji, anapiga krosi safi kabisa lakini Cannavaro anatokea na kuokoa. Inakuwa kona lakini haina matunda
MAPUMZIKO:
Dk 45+3

Dk 45, Ngoma anaanguka tena kwa mara ya tatu, anamlalamikia mwamuzi kwamba wamekuwa wakimkaba kwa siri
Dk 44, Ngoma anatoa pasi nzuri kwa Niyonzima lakini kipa JKT anakuwa mwepesi, anatoka na kuokoa mpira
Dk 41, minja wa JKT analambwa kadi ya njano kutokana na kuushika mpira kwa makusudi

Dk 39, JKT wanajitutumua kupeleka mashambulizi lakini wanaonekana kuwa na papara mara nyingi

Dk 37, Juma anaingiza krosi kwenye lango la Yanga, hata hivyo anashindwa kulenga katikati ya lango
GOOOOOOO Dk 33, Ngoma anaifungia Yanga bao safi baada ya kugongeana na Mwinyi kabla ya Tambwe kumpa pasi nzuri naye akaimalizia kiufundi kwelikweli

Dk 32, Samwel Kamuntu anajaribu tena kwa kupiga shuti kali baada ya Cannavaro kufanya kosa na mpira kuanguka karibu na mshambuliaji huyo

Dk 24 hadi 28, mpira unaonekana kuchezwa katika zaidi na Kamusoko, Niyonzima wanatawala zaidi ingawa Michael Idan wa JKT naye anaonekana kujitutumua

Dk 23, Msuva anapoteza nafasi nzuri ya kufunga bao baada ya kupata mpira wa kichwa kutokana na mpira wa kurusha wa Twite, lakini anapaisha juuuuu


Dk 21, Kamusoko anapiga faulo mbili faulo nzuri lakini inagonga mwamba na kutoka nje

Dk 17, Yanga wanafanya shambulizi tena lakini Niyonzima anachelewa kupiga. Anaangushwa na kusababisha faulo.

Dk 11, JKT wanafanya shambulizi la kwanza, Kamuntu anapiga shuti lakini linatua kwenye mikono ya Barthez.
 Dk 9, Yanga wanafanya shambulizi jingine kubwa na Kaseke anapiga shuti kali lakini mpira unadakwa na kipa ambao ulikuwa nusura umtoke.

Dk 7, Msuva anaingia vizuri na kusaidia Yanga kupata faulo karibu kabisa na eneo la kona, inachogw afaulo safi lakini inaokolewa.

DK 2 Ngoma anaingia vizuri katika eneo la hatari la Yanga, anapiga krosi safi lakini inaokolewa na kuwa kona..


KIKOSI CHA YANGA:
Bathez-1
Twitte-6
Haji Mwinyi-20
Kelvin-5
Nadir-23
Thaban kamusoko13
Msuva-27
Haruna-8
Tambwe-17
Ngoma-11
Deus Kaseke-4

SUB
Dida-30
Pato-15
Bossou-9
Telela-2
Coutinho-7
Geofrey Mwashiuya-19

Busungu-16

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic