September 19, 2015


Pamoja na kuonekana inayumba, Prisons imeibuka na kutwanga Mbeya City kwa bao 1-0.


Katika mechi ya Ligi Kuu Bara leo, Prisons imeibuka na ushindi huo baada ya kupata bao la kipindi cha kwanza.

Pamoja na juhudi za Mbeya City katika kipindi cha pili, bado mambo hayakuwa mazuri.

SHINYANGA:
Mjini Shinyanga, Stand United nayo baada ya kupoteza mechi mbili iliibuka na kuitwanga African Sports kwa mabao 2-0.

TANGA:
Baada ya kipigo kutoka kwa Simba cha mabao 2-0 ikiwa nyumbani, Mgambo nayo imeamka na kuichapa Majimaji kwa bao 1-0.


Majimaji ambayo ilikuwa haijapoteza hata mechi moja baada ya kucheza mbili na kushinda ikiwa nyumbani, imeonja utamu wa kipigo baada ya kutandikwa ikiwa ndiyo mechi yake ya kwanza ugenini, safari hii ikiwa Mkwakwani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic