Mechi imeisha na Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na kinda Kimwaga.
Dk 79, Maguli anapiga mpira wa kichwa lakini unagonga mwamba baada ya kuokolewa na Manyika
Kipa Peter Manyika naye anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Haruna Chanongo
Kuanzia dakika ya 70, Stand wanaonekana kucharuka zaidi na wamefanya mashambulizi zaidi ya matatu, mara mbili mpira unagonga mwamba katika goli la Simba.
Stand wanamtoa Selemani Selembe anaingia Elius Maguli, hata hivyo bao inaonekana Simba wanashambulia zaidi ingawa Stand nao wanajibu mshambulizi mara kadhaa
Joseph Kimwaga aliyeingia katika kipindi pili kuchukua nafasi ya Said Ndemla anaifungia Simba bao la kwanza baada ya kumchambua beki wa Stand
Kipindi cha pili cha kimeanza na mashambulizi kwa kila upande. Tutawaletea matokeo
Ni
mapumziko kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Simba na wageni wake
Stand United hakuna aliyeona bao.
Timu
zimekuwa zikishambuliana kwa zamu huku Simba wakionekana kumiliki mpira zaidi
kupitia Jonas Mkude na Mwalyanzi.
Ushindani
ni mkubwa, Stand wamekuwa wakifanya mashambulizi machache lakini yanaonyesha
kuwa makali.
Kocha
wa Stand United, Patrick Liewig anaendelea kubaki jukwaani ambako anatoa
maelezo.
0 COMMENTS:
Post a Comment