September 30, 2015

KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KILICHOIFUNGA YANGA MSIMU ULIOPITA KWENYE UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO.

MPIRA UMEKWISHAAAAAA

GOOOOOOOOO Dk 90, Msuva anapiga shuti kali, kipa anatema mpira unamkuta Ngoma anaumalizia kimiani na kuaindikia Yanga bao la pili
Dk 85 Yanga wanamtoa Tambwe na nafasi yake inachukuliwa na mshambuliaji mpya Matheo Simon
Dk 67, Mtibwa wanafanya shambulizi kali lakini Barthez anafanya kazi ya ziada, anaokoa na kusababisha kona ambayo haina matunda

Dk 63, Mtibwa wanamtoa Mohammed Ibrahim anaingia Said Bahanuzi

DK 55 hadi 59, Mtibwa Sugar ndiyo wanaonekana kupeleka mashambulizi mengi huku Yanga wakijitahidi zaidi kuzuia ili kuepusha Mtibwa Sugar kusawazisha
GOOOOOOOOO Dk 52 Malimi Busungu anaifungia Yanga bao la kwanza baada ya mabeki wa Mtibwa Sugar kujichanganya na kipa wao wakati wakiwgombea mpira na Donald Ngoma

Dk 48, kona safi ndani ya lango la Mtibwa lakini Saidi Mohammed anafanya kazi ya ziada kuokoa

Dk 47, Yanga wanapata faulo, Kamusoko anapiga shuti safi lakini linaokolewa na kuwa kona
MAPUMZIKO
KADI Dk 45+1 Telela naye analambwa kadi ya njano na mwamuzi ambaye aliamua kuzigawa sasa kama njugu
KADI Dk 45, Amissi Tambwe analambwa kadi ya njano kwa kuzozana na mwamuzi

Dk 40 hadi 44, bado inaonekana hakuna mashambulizi makali katika milando yote

KADI Dk 38, Salim Mbonde analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Busungu.

Dk 28 hadi 35, timu zinaonekana kucheza katikati zaidi kama bado kama vile zinasomana, kila upande uko makini katika upande wa safu ya ulinzi. Kwa Yanga ikiongozwa na Thabani Kamusoko na Mtibwa ni Shabani Nditi


Dk 27, Haji Mwinyi anaachia shuti lakini Said Mohammed anaokoa vizuri na kuwa kona
Dk 26, Kamusoko anachonga faulo nzuri lakini Mtibwa waokoa na kuwa kona ambayo ni ya tatu kwao, lakini haina mashara

Dk 24, Msuva anapiga kichwa safi baada ya Mtibwa Sugar kupata kona lakini Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa

Dk 19, Ngoma anawatoka mabeki wawili wa Mtibwa Sugar lakini mpira unaokolewa na kuwa kona, hata hivyo haina mafanikio


Dk 15, Rajab anawatoka mabeki wa Yanga na kupiga shuti kali, lakini mpira unapaa juu


KADI Dk 10 Selemani Rajab analambwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Cannavaro

Dk 4& 8, mpira zakdi unachezwa katikati ya uwanja, bado hakuna shambulizi kali kutoka kila upande. Ingawa Mtibwa Sugar wanaonekana kujipanga zaidi katika kiungo

Dk 2, Mtibwa Sujgar wanafika katika lango la Yanga, Yanga nao wanajibu na kuoata kona lakini haina madhara
Dk 1, Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Mtibwa, lakini si kwa shambulizi kali.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic