Ili mawazo yao yawe katika mchezo wa leo
Jumamosi na kuweza kufanya vizuri dhidi ya Nigeria, wachezaji wa Taifa Stars
tangu jana asubuhi walipigwa stop kutumia Mitandao ya Kijamii ya WhatsApp na
Facebook.
Taifa Stars inacheza na Nigeria kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam mchezo wa Kundi G kuwania kufuzu kushiriki wa Kombe la
Afrika 2017 Gabon.
Imeelezwa kuwa, Kocha wa Taifa Stars, Charles
Mkwasa, anataka wachezaji wake wote wawaze mchezo huo, vinginevyo wakitumia
mitandao hiyo, hawatakuwa makini na wanaweza kufungwa.
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Moroco,
ndiye aliyetoa agizo hilo kwa wachezaji wake jana asubuhi katika mazoezi ya
mwisho ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, akiwasisitiza huduma ya mtandao wa
‘internet’ (data) katika simu zao.
“Zimeni
data, mnatakiwa mpate muda mwingi wa kupumzika huku akili zenu mkizielekeza
katika mechi ya kesho (leo), hivyo hamtakiwi kutumia WhatsApp hata Facebook.”
Wakati huohuo, kocha mshauri wa Taifa Stars,
Abdallah Kibadeni, amesema: “Watanzania wasiwe na wasiwasi kwa mchezo huu,
vijana wetu wapo vizuri, waje tu kuwashangilia uwanjani.”
0 COMMENTS:
Post a Comment