Katika kuhakikisha timu yake inatumia vyema mipira ya adhabu ya penalti, kipa wa
Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’, ameomba kupiga penalti zote zitakazotokea ndani
ya uwanja.
Kauli hiyo,
aliitoa mara baada ya kiungo mkabaji wa timu hiyo, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko
kukosa penalti katika mechi dhidi ya Azam FC iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1
i kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, juzi Jumamosi.
Huyo siyo
mchezaji wa kwanza kukosa penalti kwenye timu hiyo, timu hiyo kwenye michuano
ya Kagame iliwahi kukosa penalti tatu kwenye mechi mbalimbali, pia ilitolewa
kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na Azam kwa njia ya penalti.
Barthez alisema kuwa anashindwa kuelewa tatizo walilonalo
na kusababisha washindwe kutumia vyema nafasi za penalti katika kufunga mabao.
Barthez alisema,
kocha wao katika mazoezi kila siku hutoa programu kwa wachezaji wote jinsi ya
kupiga penalti, hivyo anashindwa kuelewa sababu ya kushindwa kupiga kwenye
mechi.
Aliongeza kuwa,
yupo tayari kupiga penalti zote zitakazotokea uwanjani kama kocha wake
atamruhusu, anaamini ana uwezo mkubwa wa kupiga na kufunga.
“Kama kufundishwa
tunafundishwa kila siku na kocha wetu na wachezaji wanapiga na kufunga.
“Sasa nashindwa
kuelewa tunapopata penalti wachezaji wanakosa, mimi nafikiri wachezaji
wanashindwa kujiamini, hasa pale mtu anapoambiwa aende akapige penalti.
“Mimi ninaomba
nipige penalti zote tutakazozipata, ninaamini nina uwezo mkubwa wa kupiga
penalti,” alisema Barthez.
Pluijm alipotakiwa
kuzungumzia hilo, alisema: “Mchezaji yeyote anaruhusiwa kupiga penalti pale
inapotokea, kikubwa anachotakiwa ni kujiamini kabla ya kwenda kupiga.”
0 COMMENTS:
Post a Comment