October 9, 2015


Televisheni ya Azam TV, nao wamejitokeza kudhamini sherehe ya kumuaga Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete iliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa).

Sherehe hizo zimepangwa kufanyika Jumatatu ijayo kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mweyekiti wa Taswa, Juma Pindo amesema kuwa Azam TV, wamedhamini sehemu ya zawadi za ving’amuzi vya Televisheni hiyo vitakavyotolewa kwa wanamichezo bora 10 waliofanya vizuri katika kipindi chake.
Sherehe hizo zitakazopambwa na burudani mbalimbali wakati wa sherehe hiyo ambayo zaidi ni maalum kumshukuru Kikwete ambaye alionyesha uanamichezo wakati wa kipindi chake cha uongozi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic