February 7, 2021

 


CEDRIC Kaze,Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga amesema kuwa haoni tatizo ya mechi yao dhidi ya watani wa jadi Simba kubadilishwa tarehe na Bodi ya Ligi Tanzania.

Awali mechi hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa shauku kubwa na wadau wa masuala ya soka ndani na nje ya Bongo ilitarajiwa kuchezwa Februari 20.

Ila kwa sasa rasmi mechi hiyo imebadilishwa tarehe na itapigwa Mei 8,itakuwa ni ya mzunguko wa pili msimu wa 2020/21.

Ile ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Mkapa zama za Sven Vandenbroeck ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na vigogo hao waligawana pointi mojamoja.

Kaze amesema:"Sioni tatizo la mechi kupelekwa mbele kwani hilo limetokea na sitaweza kubadili kwa kuwa ni ratiba nina amini itafika na tutacheza ila kwa sasa acha tuweke nguvu kwenye mechi zetu zilizo mbele yetu,"

Februari 13, Yanga itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu ugenini mbele ya Mbeya City ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

Ule wa kwanza Uwanja wa Mkapa, Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 44 ilishinda bao 1-0 lililopachikwa na Lamine Moro hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa Uwanja wa Sokoine. 

11 COMMENTS:

  1. Ni bora kuahirishwa ili mpate muda zaidi wa kujitayarisha hasa kwa vile mechi ya jana ya daraja la kwanza African Sport kuondoa bikira nao wakiwepo ugenini wakiwemu minyota ya mabilioni tuliowatarajia ndio wataouleta ubingwa ambao umeshahakikishwa. Hayo ni matokeo ya kutokana na vitendo vyenu sio vya uungwana vya kuchoma moto jezi ya Mnyama mbali na vitondo vingi vya hapo mwanzo nanyi kila mkiwafanyia uovu mnaowaita mikia ndio kwao kuzidi kushamiri kwasabau ya usafu wa roho zao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ujui hata kuandika ndio mbumbuu za Rage anazosema wewe

      Delete
    2. huyu bwege kaandika nini mbona haeleweki!!!!!yaonekana shule hamna humo.weeee kaa kuhesabu mechi ya kirafiki ya yanga unaacha kujiuliza madhara ya kutoka droo na azam jana.

      Delete
  2. Tangu mumejiita tff fc munajipangia tu mutakavyo kila kukicha mukicheza na yanga tu mpaka muwaulize paka wenu acheni ushamba munaharibu sana ratiba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo bongo ushabiki tumeweka mbele, As Vita na Tp Mazembe game zao za jana jumamosi na leo zimeahirishwa kwa ajili ya mechi za kimataifa. Kama mnataka gomeni kucheza muisubiri hiyo mei halafu muendelee

      Delete
  3. TFF hii siku zote inasubiria matakwa ya Paka FC, ndio maana hata wachambuzi walishasema hii dani itabadilishwa kwasababu wanajua aina ya Viongozi wa TFF wa Sasa.

    ReplyDelete
  4. Kwa hamuoni jinsi rativa ilivyokuwa tight kwa upande wa simba? Hivi kweli hakukuwa na genuine reason au tumezoea tuu kulaumiana? Kipindi hiki hata flights tuu ni shida, huenda hilo nalo limechangia

    ReplyDelete
  5. Hata hivyo haya mabafiliko yatawasaidia yanga ili wajipange zaidi maana kipindi hiki ni kama wamevurugwa. Na African Sports ndio kachomoa betri kabisaaaa

    ReplyDelete
  6. Utopolo hamna chochote, mmsikilize mume wenu la sivyo tutawapa takaka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic