OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa anaamini watani zao wa jadi Yanga, wana stress, (presha) kutokana na kuona timu hiyo ikifanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na kuingia mikataba mbalimbali.
Kumekuwa na majibizano kwenye mitandao ya kijamii kati ya Ofisa Habari wa Simba, Manara kuhusu namna hali yake ya utani ilivyo kwa mashabiki wa Yanga ambapo alipandisha picha kwenye mtandao wa kijamii ukiwa na jezi ya Yanga pamoja na Simba.
Baada ya Manara kupandisha jezi hizo mashabiki ambao inaaminika ni wa Yanga walitoa maoni yao wakimponda Manara kutokana na jambo hilo huku wakiamini kwamba ni utani uliopitiliza.
Kupitia kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Februari 6, Manara amesema:-"Msemaji wao aliwahi kusema kuwa jezi ya Simba ni takataka, hazifai hatakufutiwa viatu je mliskia Simba tukilalamika?
"Hatujawahi Simba kulalamika, pia hivi karibuni jezi ya Simba iliweza kuchomwa moto.Watu walishangilia lakini hakuna aliyesimama kuzungumzia hili pia.
"Sasa vipi hawa Yanga wanakuaje, wanalalamika kwa nini?Simba mliwahi kuskia wanalalamika. Sasa vipi Yanga ninachokiamini ni stress za matokeo, stress za kuona Simba Super Cup imefanikiwa, stress za kuona Simba inatwaa ubingwa mara ya nne.
"Stress za kuona Simba inatinga hatua ya robo fainali ndio katika hili hakuna matatizo inafanikiwa, stress za kuona Simba inaingia mikataba kila kukicha," .
Pia Manara amesema kuwa anaamini kuwa wanachama wa Klabu ya Simba kesho watafanya maamuzi sahihi kwenye uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti iliyoachwa wazi na Sued Mkwabi aliyebwaga manyanga.
Wagombe ambao wanawania nafasi hiyo ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu.
No comment
ReplyDeleteManara yupo sahihi kabisa Yanga waache kupanic. Nadhani Kama kuna kitu kibaya zaidi kilipaswa kulaaniwa na kila mzalendo mtanzaniia. kulaaniwa na kila kiongozi wa nchi hii. Kulaaniwa na kila mpenda michezo wa nchi hii. Kulaaniwa na hata na viongozi wa Yanga ni pale Mashabiki wa Yanga walipokwenda uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kuwapokea wapinzani wa Simba timu ya pleateu fc kutoka Nigeria. Mashabiki Yanga wamekuwa sio kushabikia na kufanya utani kwenye mechi za kimataifa za Simba tu, la hasha.Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakishiriki kuzisaidia timu ngeni kuhakikisha Simba inapoteza mechi hapa nyumbani na katika hili Ushahidi upo wa maneno na vitendo kwa ushahidi wa picha za video kabisa. Sasa huu utani wa Haji manara wa kidimbwi Kama kidimbwi Cha maji au hata kama hicho kidimbwi chengine kisichowekwa bayana sifikirii Kama Kuna tatizo kuliko hujuma za wazi wanazozifanya Mashabiki wa Yanga zidi ya mechi za simba kimataifa.
ReplyDeletePanic gani wakati tumeanza kukusanya..au mmeshasahau?
ReplyDeleteYeye Manara mambo ya utani anayapenda. Lakini akitaniwa yeye kisawasawa anapaniki vibaya ataanza kumwomba Rais amvue mtu cheo mtu. Anaomba huruma ya nchi nzima. Na alishaahidi atabaki kuwa msemaji wa Simba tu na hataitaja Yanga lkn leo amesahau yote. Lkn ajue watu wanamvutia kasi
ReplyDeleteKama sasa hivi yupo tayari kwa utani atuambie tumkaribishe hadharani Mhe.
ReplyDeleteHuyo mheshimiwa wenu hajui utani alitaniwa na Manara akapaniki Mara sijui mi naishi Mbezi Nina mke mzuri kwa kifupi Manara kwenye utani wake huwa aongelei maisha ya mtu binsfsi anaitania Yanga Sasa Jerry Muro yeye anamuongelea Manara kwa maisha yake binsfsi kitu ambacho so sahihi,na sio Jerry Muro washabiki wote wa Yanga utani hawajui Wana STRESS
DeleteMbamtisha nani ninyi utopolo sana sana mnachojua ni matusi tuu, utani hamuwezi
ReplyDeleteHivi manara Bila kuitaja taja YANGA Hupati Afya?
ReplyDeleteHana lolote ndomana amebaki kuitaja yanga maisha yake yote
DeleteJamaa cjawah kumuelewa kwani usemaji wake lazima aitaje Yanga
Kama ckuiogopa ukoo.
Jerry Muro alivyokuwa Kila akiongea anaitaja Simba na kuitania na yeye alikuwa anaiogopa toka lini Manara akaiogopa Yanga kwa kitu gani hasa ukizungumzia hata Sasa hv Simba wacheze na Yanga timu itakayopewa nafasi kubwa ya kushinda ni Simba ukiondoa kwamba dabi Ina matokeo yoyote,Ila ndugu zetu ki ukweli wamepaniki na Haji Manara ndiye adui yao mkubwa wengi wasiojua utani wa jadi wanamchukia na ndio wengi ambao hawajui Mpira na ndo hao wanaofikiri Yanga ndio timu iliyoleta Uhuru wa Tanganyika,Yanga timu ya Serikali,Mara sijui timu ya wananchi Yani walikuwa wanajiona wao ndo Wana stahili kuchukua ubingwa wa Tanzania na kwa kiasi Fulani walifanikiwa mpaka Leo wanajiita mabingwa wa kihistoria ingawa mi siamini Kama kwa Mpira wa uwanjani Bali ni kutokana na Aina ya viongozi wa chama cha Mpira wengi walikuwa wakiipendelea Yanga waziwazi kwenye mwamuzi mengi.
DeleteSimba ni lazima waitaje Yanga ndo maana ya kuitwa watani wa jadi.Ni mtu mlemavu tu ndo atakuwa haelewi. Kumbukeni mwaka 1989 Simba ilikuwa ishuke daraja lakini Yanga ikakubali kuinusuru.Huo ndo utani wa jadi.leo kwangu kesho kwako.
ReplyDelete