February 7, 2021

 


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa kichapo cha bao 1-0 walichokipata mbele ya African Sports Februari 6 ni sehemu ya mchezo.


Ikiwa Uwanja wa Azam Complex kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports safu ya ulinzi inayoongozwa na Lamine Moro iliokota wavuni bao dakika ya 73.


Kipa namba moja Metacha Mnata haikuwa na chaguo baada ya mshambuliaji wa African Sports,  Adam Uledi kutupia bao la ushindi.


Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 90 licha ya Yanga kupambana kusaka ushindi ikiwa na nyota wao mpya, Fiston Abdulazack ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya ENPPI.


Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa vijana wake walitengeneza nafasi nyingi ila walishindwa kuzitumia jambo ambalo watalifanyia kazi.


"Ni mchezo wa kirafiki ipo wazi, matokeo ya kufungwa hayatabadilika ila tumejifunza jambo na wachezaji pia wameonyesha juhudi ni sehemu ya matokeo,".

12 COMMENTS:

  1. Piston tuliyoitegemea imeshindwa kufanya kazi na kulikwamisha gari kukosa tahsruki kwa mara ya kwanza tena basi ndani ya nyumba yetu na huku Mnyama akizidi kuchonga makucha yake na kukata mbuga

    ReplyDelete
  2. Kaanbulia teke kutoka kwa wageni wake ndani ya nyumba yake. matokeo ya Majigambo yaliyopundukia mipaka

    ReplyDelete
  3. Mpira ndio ulivyo, tupunguze maneno maneno tufanye kazi. Pia jazba sio kitu kizuri

    ReplyDelete
  4. Nisikie tena..,YOONGOO ndo timu pekee haijawah kufungwa duniani kwa mwka 2021

    ReplyDelete
  5. Nafasi ya fiston Bora angecheza mwakalebela huenda tungepata matokeo

    ReplyDelete
  6. African sport Hongera kwakumbikiri utopolo na Sasa tutjitobolea tu tutakavyo

    ReplyDelete
  7. Kila mchezaji lazima atakuwa na jukumu la kufanya kazi iliyomleta Yanga, huyo Fiston namjua vizuri, lakini lazima aendane na mfumo sahihi wa timu anayocheza kwa sasa, ndiyo maana nasema nitajua baada ya hizi mechi za kirafiki.

    ReplyDelete
  8. Kiporo karibu kichache asilimia 100.. hehehe..mikia aka paka mweusi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic