October 15, 2015

Kikundi cha Jakaya Sanaa kilichoibuka bingwa wa shindano la Ngoma za Asili kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 yanayoendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa ya Vita vya Majimaji, Songea.



Mmoja wa Wanakikundi cha Jakaya Sanaa, akipokea zawadi ya fedha taslim, medali ya dhahabu na cheti kama bingwa wa shindano la Ngoma za Asili katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 linaoendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.


Wasanii wa Kikundi cha Lihanje kutoka Kilagano- Ngoma ya Kioda wakionyesha manjonjo yao katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2015 linaoendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

Kikundi cha Ngoma cha Lihanje-Ngoma ya Mganda wakifanya yao katika Shindano la Ngoma za Asili kwenye tamasha la Majimaji Selebuka 2015.

Mkurungenzi mwenza wa Asasi ya Somi, Dk Damas Ndumbaro wa pili kutoka kushoto akifuatilia kwa ukaribu Shindano la ngoma za asili katika tamasha la kila mwaka la Majimaji Selebuka 2015 kwenye Uwanja wa Makumbusho wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

aji Mkuu katika Shindano la Ngoma za Asili, Balthazar Namusya akimvisha medali ya shaba mkuu wa Kikundi cha Ngoma cha Lihanje Ngoma ya Kioda kilichoshika nafasi ya tatu kwenye Tamasha la Majimaji Selebuka.

Wasanii kutoka vikundi vitatu tofauti vilivyofanikiwa kuingia fainali ya shindano la Ngoma za Asili katika tamasha la majimaji selebuka wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutunukiwa zawadi zao. Tamasha hilo linaendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, Songea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic