October 15, 2015


Promota wa ngumi za kulipwa nchini, Jay Msangi amesema maneno haya baada ya ile tuzo yake aliyosawadiwa na Taswa.

“Natoa shukurani kubwa kwa Chama cha waandishi wa habari za Michezo Tanzania (Taswa)kwa kutambua mchango wangu katika kukuza mchezo huu pia katika mazungumzo yangu nilimuahidi Rais kuendeleza zaidi ya hapa.

“Kama mnvyofahamu mwanzoni mwa wiki hii Taswa walinipa Tuzo ya promota aliyeinua mchezo huu katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete anayetarajiwa kumaliza muda wake mwezi huu.


“Nimefarijika sana kuona Rais wa nchi yangu anatambua thamani yangu katika kukuza mchezo huu licha ya wengine kunibeza ila inatosha kama Rais wa nchi yangu anatambua na kuthamini mchango wangu basi  it's enough.

“Katika mazungumzo yangu na Rais nimemwahidi kutomwangusha licha ya kumaliza  muda wake madarakani pia sitowangusha mashabiki wa masumbwi Tanzania na nitaendelea kuwaletea mapambano mkubwa ya kimataifa  wajiandae kwa  Desemba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic