October 15, 2015


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amefikisha umri wa miaka 60, leo.

Kiongozi huyo wa Simba amekuwa akiwatia tumbo joto watani wake Yanga hasa kuhusiana na kusema anawaandalia supu ya mawe na kachumbari ya miiba.
Hata Yanga ilipoifunga Simba kwa mabao 2-0 na kuonekana kuanza kufuta uteja, karibu kila shabiki wa Yanga alikuwa akimtaja Hans Poppe ambaye amekuwa akiwaacha tumbo joto.
Hans Poppe amefikisha umri huo na sasa yuko Iringa ambako amejumuika na familia yake kusherekea miaka 60 ya kuzaliwa.

“Niko Iringa nimejumuika na watoto na familia kwa ujumla,” alisema Hans Poppe ambaye ni askari mstaafu ya jeshi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic