Na
Saidi Msumi, aliyekuwepo
Morogoro
Mzunguko
wa tano wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 uliendelea tena
katikati ya kwa michezo mitatu ambapo katika Uwanja wa Taifa Simba waliwakaribisha
Stand United ‘Chama la Wanna’. Azam walivaana na Coastal Union wakati kule
mjini Morogoro kulikuwa na kivumbi kati ya wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar
dhidi ya mabingwa watetezi Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Makala
yangu siku ya leo nitaangazia mchezo namba 35 Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga,
mwamuzi akiwa ni Erick Okoka kutoka Arusha.
Sitalenga
masuala ya kiufundi sana, badala yake ninaangalia usalama wa wachezaji uwanjani
pale.
Mara
nyingi nimekuwa nikilalamikia usalama wa mashabiki na mali zao hasa katika
uwanja mkuu wa taifa pale klabu Simba na Yanga zinapokutana. Kumekuwa na usalama
mdogo wakati wa kutoka mara mchezo unapokwisha na kufanyika vitendo vya wizi na
unyang’anyi kwa mashabiki lakini afadhali sasa kidogo ulinzi unaridhisha
kidogo.
Tuanze
kuutazama mchezo kati ya Mtibwa sugar na Yanga ambapo baada ya mwamuzi Erick
Onoka kupuliza filimbi kuhitimisha mchezo huo asilimia kubwa ya mashabiki
wakaanza kuingia uwanja kushangilia ama hakika ilikuwa tafrani sio kwa
wachezaji wala kwa waandishi wa habari ambao walikuwa wanawataka kufanya
mahojiano na wachezaji au makocha wa kila timu hali ilikuwa ngumu kwa kweli.
Hili
suala la mashabiki wa soka kuingia uwanjani si suala la kwanza kutokea katika Uwanja
wa Jamhuri na hata Uwanja wa CCM mkwakwani ambapo kumekuwa na kasumba hii ya
mashabiki kuingia uwanjani hasa pale mchezo unapomalizika.
Kwa
baadhi ya watu wanaweza wakakuambia ni furaha na mapenzi waliyonayo kwa wachezaji wao lakini huwezi kujua dhamira ya
kila mtu kama kweli ana mapenzi na hiyo timu labda anataka kumdhuru tutajuaje?
Au
hajaridhishwa na maamuzi ya mwamuzi na anataka kwenda kumdhuru? Mie nadhani
sasa suala hili si la kufumbiwa macho hata kidogo ipo siku tutakuja kushuhudia
wachezaji wakiwa wamejeruhiwa kutokana na tabia hii ya kijinga ya kuingia
uwanja lakini pia inakuwaje walinzi mnaruhusu watu wasiohusika kukaa ndani ya
uwanja?
Inatupasa
sasa kuacha kujuana na sheria kufuata mkondo wake mana hakuna mtu aliyejuu ya sheria
huku chini wabaki wanahabari na walinzi kuliko kuwa na mkusanyiko mkubwa ambao
baadae unaanza kuingia uwanjani bila ya sababu ya msingi.
Pia
tabia hii pia ipo kwa baadhi ya watu hasa vijana wadogo katika uwanja mkuu wa
taifa ambao utawakuta wamejazana sehemu ya kutokea wachezaji hasa wakiwaomba
jezi au viatu?Huu nao ni usumbufu mwingine kwani huwezi kumtafuta sehemu
nyingine ili umuombe hivyo vitu mie nadhani sasa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) pamoja na vyombo vyenye mamlaka ya ulinzi na usalama vianze kutolea macho
masuala haya kwa ukaribu wake mapema ndio mana nakukumbusha Rais wa TFF, Jamal
Malinzi tusije tukaunda tume ya bure
kabisa baadae huko kuchunguza endapo tatizo litatokea uwanjani.
Nawasilisha kwa leo.
0564-234573
0 COMMENTS:
Post a Comment