October 1, 2015

KIKOSI CHA MBEYA CITY KILICHOIVAA TOTO AFRICAN MJINI MWANZA, LEO.
Mbeya City imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Toto African katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo.


Wageni Mbeya City ndiyo walianza kupata bao katika dakika ya 12 kupitia John Kabanda aliyefunga kwa mkwaju wa penalti. Bao hilo likadumu hadi kipindi cha kwanza kilipoisha.

Kipindi cha pili kilionekana ni cha Mbeya City ambao walitawala zaidi, lakini wakapoteza nafasi nyingi za kufunga.

Toto waliibuka na kuanza kusukuma mashambulizi mengi zaidi kuanzia dakika ya 70 na kuonyesha kuwachanganya wageni wao.

Edward Christopher aliipatia Toto bao la kusawazisha kwa shuti kali la kushitukiza lililomshinda kipa mkongwe Juma Kaseja na kaundika bao hilo.

Kaseja na Edo, wote waliwahi kuwa wachezaji wa Simba kabla ya kila mmoja kuchujua njia yake.


Mbeya City ilicheza bila ya nahodha wake ambaye amefungiwa miaka miwili baada ya kumdhalilisha nahodha wa Azam FC, John Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic