NGOMA (KATIKATI) AKIPAMBANA NA SHOMARI KAPOMBE NA AGGREY MORRIS |
Mshambuliaji nyota wa Yanga, Donald Ngoma na Juuko Murshid
wa Simba watajadiliwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
baada ya kutuhumiwa kufanya makosa kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
Simba na Mbeya City zimeshawasilisha malalamiko
yao muda mrefu hivyo kilichobaki ni kamati hiyo kuketi na kutoa ufafanuzi.
JUUKO |
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB),
Boniface Wambura amesema makosa yaliyofanywa na wachezaji hao ni ya kinidhamu
hivyo yatajadiliwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Alisema kuwa makosa hayo ni makubwa na hayawezi
kuamuliwa na Kamati ya Uangalizi ya Matukio ya Ligi ya saa 72, hivyo yataamuliwa
kwenye kamati ya nidhamu.
“Makosa waliyofanya wachezaji hayo ni ya
kinidhamu yapo kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF, wao watatoa uamuzi,” alisema
Wambura.
Kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu kuhusu
Ngoma kutojadiliwa na kamati hiyo kwani malalamiko dhidi yake yaliwasilishwa
TFF muda mrefu.
0 COMMENTS:
Post a Comment