MWAMWAJA... |
Kocha wa zamani wa Simba na Prisons, David
Mwamwaja, anatarajiwa kufanyiwa kipimo cha CT Scan kutokana na kuumia vibaya
kichwani baada ya kuanguka hivi karibuni.
Mwamwaja ambaye kwa sasa ni kocha wa Mji
Njombe, juzi Alhamisi alifanyiwa upasuaji wa kichwa katika Hospitali ya
Muhimbili jijini Dar alikolazwa kutokana na matatizo hayo.
Mke wa kocha huyo, Maria Mwamwaja, alisema
Mwamwaja anaendelea vizuri tofauti na awali na sasa atafanyiwa vipimo zaidi
kwenye kichwa chake ili kubaini na kutibu kabisa tatizo linalomkabili.
“Baada ya kufanyiwa upasuaji sasa anaendelea
vizuri japokuwa anatakiwa kufanyiwa kipimo cha CT Scan ambacho kinahitaji
fedha, hivyo tunawaomba wadau waendelee kutoa michango kufanikisha matibabu
yake,” alisema mama huyo.
Kwa wale wanaotaka kumchangia kocha huyo,
watume michango yao kupitia namba ya mkewe, Maria Benjamin Mwamwaja,
0714 621 554.
0 COMMENTS:
Post a Comment