October 2, 2015


Pamoja na kufunga bao katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amewalaumu mabeki wa Mtibwa waliokuwa wakiongozwa na Salim Mbonde, kutokana na kumchezea kibabe na kumpiga rafu za makusudi.


Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Ngoma kucheza nje ya Dar katika ligi kuu, alisema alishindwa kucheza vizuri kutokana na mabeki hao kumpania na kumchezea vibaya.
 
MBONDE AKIMTHIBITI NGOMA...

Mpaka dakika ya 90, mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe alikuwa hajapiga shuti lolote golini, lakini aliwaliza Mtibwa baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Mtibwa, Said Mohammed katika dakika za lala salama.

“Uwanja tuliochezea kwa kweli ni mbovu hasa sehemu ya kuchezea (pitch), ilikuwa ikinipa shida mwanzoni lakini nilijitahidi kuizoea.

“Mabeki wa Mtibwa nao walifanya mambo mengi ili wanitoe mchezoni lakini ilishindikana kwa kuwa nilitambua umuhimu wa mchezo na sikutaka kuwaangusha mashabiki ambao wamesafiri kutoka sehemu mbalimbali mpaka hapa (Morogoro) kuja kutupa sapoti.

“Lakini siyo kwamba wapinzani walikuwa wabaya, isipokuwa mabeki wao walionekana kutukamia na mara kadhaa wameniangusha kwa kunicheza faulo za makusudi lakini kizuri ni kuwa tumeshinda,” alisema Ngoma ambaye mpaka sasa amefunga mabao manne katika ligi kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic