November 2, 2015


Uongozi wa Simba hivi sasa upo katika harakati mbalimbali za kutaka kukiimarisha kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri zaidi katika mechi zake za Ligi Kuu Bara msimu huu.

Ili kuhakikisha hilo linatimia, baadhi ya viongozi wa timu hiyo wameshaingia mitaani kusaka wachezaji wenye uwezo mkubwa watakaowasajili katika kipindi cha dirisha dogo litakalofunguliwa Novemba 15, mwaka huu.

Wachezaji ambao majina yao tayari yameshafikishwa katika kamati ya usajili ya timu hiyo ni pamoja na lile la mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho, lakini jina hilo kabla halijajadiliwa na kamati hiyo, hofu kubwa imetawala miongoni mwa viongozi hao.

Hofu hiyo si nyingine, bali ni ile inayohusiana na mshahara ambapo wamedai kuwa endapo watamsajili mchezaji huyo basi wataingia gharama kubwa zaidi ya kumlipa fedha nyingi ambazo baadaye zinaweza kuwasababishia matatizo.

Kutokana na hali hiyo, Rais wa Simba, Evans Aveva, amesema kuwa, itabidi wampotezee mchezaji huyo japokuwa ni mzuri na ana uwezo mkubwa wa kucheza soka.

“Tumeshaanza harakati za kusaka wachezaji ambao tutawaongeza katika kipindi cha dirisha dogo la usajili lakini kuhusiana na Coutinho sidhani kama tutamsajili.

“Atatugharimu fedha nyingi sana kwani atataka mshahara mkubwa ambao hatutaweza kumlipa, hivyo kutokana na hali hiyo, hatuwezi kumsajili lakini pia hatutaki mchezaji kutoka Yanga kwa sasa,” alisema Aveva.


Yanga inadaiwa kumlipa Coutinho mshahara wa dola 2,500 kwa mwezi, sawa na shilingi 5,000,000.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic