November 7, 2015


Azam FC inaendesha mambo yake kama timu za Ulaya hasa England, kwani baada ya kukataa straika wake Didier Kavumbagu kujiunga na Simba kwa mkopo, imemruhusu nyota huyo kwenda Sweden.

Mtu wa karibu na Kavumbagu amesema straika huyo raia wa Burundi amepata timu Sweden na Azam imekubali kuondoka kwake na sasa inatafuta mbadala wake klabuni.

Kocha wa Azam, Stewart Hall, alikataa Kavumbagu kujiunga na Simba kwa mkopo kwa kile kilichodaiwa kutotaka kujiongezea timu pinzani katika ligi huku akionekana kuruhusu mchezaji huyo kujiunga na Yanga.
Kavumbagu anaonekana hana furaha ndani ya Azam kutokana na kutokuwa na uhakika wa nafasi kikosi cha kwanza, sasa anakwenda Sweden alipo straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi.

Hall amesema kuwa: “Imekuja ofa hapa Kavumbagu anatakiwa na timu moja ya Sweden yeye pamoja na Farid Mussa na Mudathir Yahya, hatuna jinsi sasa tunatafuta mbadala wa Kavumbagu.”

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba alipotafutwa alisema: “Bado ofa hiyo haijafika kwangu, ila kama imekuja nitaiona tu na labda niseme hatuna pingamizi kwa Kavumbagu kama anataka kuondoka, muhimu ni makubaliano tu.”

Siku za nyuma gazeti hili limewahi kumnukuu Kavumbagu akisema kwamba, yupo tayari kuondoka Azam ili kwenda timu nyingine ambako atapata nafasi ya kucheza. Straika huyo kwa sasa yupo kwao Burundi anaitumikia timu ya taifa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic