KERR AKIWA NA SALEH ALLY MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA KAMBI YA STARS |
Na Saleh Aly, Johannesburg
Kocha
wa Simba, Dylan Kerr leo ametembelea kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars jijini hapa.
Stars imeweka kambi kujiandaa na mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Algeria ambayo itapigwa Novemba 14 jijiji Dar es Salaam.
Kerr
ametua katika kambi ya Stars na kusema amekuja kuiunga mkono Stars pia kuwaona
wachezaji wake.
“Najivunia
wachezaji wangu walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars. Lakini niko hapa
kuiunga mkono Tanzania kwa ujumla na wachezaji wote kwa kuwa ikifanya vizuri ni
sehemu ya mafanikio ya Simba,” alisema Kerr.
Kerr
alionekana mchangamfu, alizungumza na wachezaji mbalimbali lakini akaIsisitizia
SALEHJEMBE kwamba Tanzania ina nafasi ya kufanya vizuri na inachotakiwa ni
kujiamini.
0 COMMENTS:
Post a Comment