Na Mwandishi Wetu, Johannesburg
Kikosi
cha Taifa Stars leo kitapumzika kwa siku moja baada ya mazoezi ya siku sita
mfululizo.
Kocha
Charles Boniface Mkwasa ameamua vijana wake wapumzike kabla ya kufanya mazoezi
mengine kesho katika Uwanja wa Edenvale jijini Johannesburg.
Baada
ya mazoezi ya kesho, Stars itakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa
ya Afrika Kusini chini ya miaka 23 itakayopigwa Jumanne.
“Mapumziko
ni Jumapili, pia wachezaji watapata muda wa kutembea kidogo hapa na pale. Baada
ya hapo tutarejea tena mazoezini Jumatatu,” alisema Mkwasa.
Stars
inajiandaa na mechi dhidi ya Algeria kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018 nchini
Urusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment