MADKTARI WAKIMHUDUMIA TSHABALALA |
Beki
wa pembeni wa Taifa Stars, alipumzishwa kwa muda baada ya kugongana na
mwenzake.
Tshabalala
ambaye ni beki wa Simba ni kati ya wachezaji walio katika kambi ya Taifa Stars
hapa jijini Johannesburg.
Baada
ya kugongana na mwenzake, madaktari wote wawili walio hapa kambini walimfanyia
uchunguzi na kuona yuko katika hali nzuri.
Lakini
alipumzishwa kidogo na kesho anatarajia kuendelea na mazoezi na wenzake kwa
kuwa leo timu haikufanya mazoezi baada ya mapumziko ya siku moja tokea itue
hapa siku sita zilizopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment