Na Saleh Ally, Johannesburg
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa jana
aliungana na baadhi ya wataalamu wa masuala ya soka nchini hapa kuangalia
baadhi ya mechi za Algeria.
Stars inajiandaa kuivaa Algeria Novemba 14 jijini Dar es Salaam
katika harakati zake za kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Mkwasa aliamua kufanya hivyo akiungana na baadhi ya memba wa
benchi la ufundi kama Abdallah Kibadeni na Juma Mgunda, kuangalia namna Algeria
wanavyopambana.
Mkwasa akiwa na memba hao na baadhi ya wataalamu wa soka Afrika
Kusini walioalikwa, waliangalia pamoja.
“Tunaangalia kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali. Soka ni
mchezo wenye mambo mengi ikiwa ni pamoja na kujifunza kupitia kwa wenzako.
“Lengo ni kujua Algeria wana mipango ipi, mfano tofauti ya
mipango ya nyumbani na ugenini na nini cha kufanya,” alisema.
Stars jana ilifanya mazoezi mara mbili kwenye Uwanja wa Edenvale
jijini hapa ikiwa ni sehemu ya kuendelea kujifua.
0 COMMENTS:
Post a Comment