November 6, 2015


Aliyekuwa Kocha wa viungo wa Simba, Dusan Momcilovic ‘Dule’ raia wa Serbia, amepata dili ambapo sasa anainoa timu ya OFK Beograde inayoshiriki Ligi Kuu ya Serbia.

Hata hivyo wakati akiondoka, Dule alisema lazima Simba itafungwa na Yanga katika mchezo wake uliokuwa unafuata.


Dule aliyeondoka nchini mwishoni mwa Oktoba, mwaka huu, alikuwa ana kazi maalum ndani ya kikosi cha Simba ya kuwajengea stamina wachezaji wa timu hiyo, kazi aliyoifanya kwa miezi mitatu kabla ya mkataba wake kumalizika mwezi huo.

Akizungumza kutoka Serbia, Dule alisema mara baada ya kumalizana na Simba, alirejea nyumbani kwao ambapo kwa siku chache tangu afike huko akapata dili hilo.

“Kuna mpango mwingine wa kwenda kufundisha nje ya nchi hii, ikiwa tayari nitatoa taarifa. Nimesikia chinichini mipango ya Simba kutaka kunirudisha japo sijapata rasmi kauli kutoka kwa viongozi wa Simba, lakini kama wakinihitaji na tukakubaliana vizuri basi nitarudi,” alisema Dule.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic