Na Saleh Ally, Johannesburg
KIKOSI cha Taifa Stars kilichoweka kambi nchini hapa
kimeandaliwa mpishi maalum.
Pamoja na ubora wa hoteli ya Holiday Inn waliyofikia, lakini
Stars wamewekewa mpishi huyo.
Mratibu wa Taifa Stars, Msafiri Mgoyi amesema lengo ni
kuhakikisha wachezaji wanakula chakula sahihi na wanachohitaji.
“Wakati mwingine hata chakula ni utamaduni. Lakini mpishi
anayekuja hapa ni yule ambaye anajua kupiga hata ugali.
“Wachezaji watakula wanachotaka na kwa wakati mwafaka. Kingine
bado ni umuhimu wa suala la usalama,” alisema Mgoyi.
Stars inajiandaa kuivaa Algeria Novemba 14 jijini Dar es Salaam
katika harakati zake za kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Kikosi hicho chini ya Charles Boniface Mkwasa kinahitajika
kushinda mechi ya kwanza na kujiwekea mazingira mazuri kabla ya mechi ya pili
Novemba 17, ugenini.
Kikosi cha Taifa Stars kimefanya
mazoezi leo Asubuhi, pia kitaendelea kufanya jioni.
Mazoezi yamefanyika chini
ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye ana wasaidizi wengine kama Hemed
Morocco na Juma Mgunda pia mshauri wa masuala ya Ufundi, Abdallah Kibadeni
pamoja na Kocha wa Makipa, Manyika Peter.
Meneja ni Omary Kapilima.
Mazoezi yamefanyika kwenye
Uwanja wa Edenvale kwenye kitongoji cha Edenvale jijini Johannesburg, Afrika
Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment