Kocha
Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameamua kumalizia mapumziko yake jijini dar
es Salaam.
Wakati
Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kwa takribani wiki mbili, Pluijm amesema ataendelea
kubaki jijini Dar es Salaam.
“Nitakuwa
Dar es Salaam na familia yangu, pia nitaendelea na mipango kwa ajili ya
maandalizi ya ligi,” alisema.
Awali
kulikuwa na taarifa, Pluijm angerejea Ghana kwa ajili ya mapumziko ya
kifamilia.
Yanga
iko katika nafasi ya pili ikiwa na point 23 nyuma ya Azam FC yenye pointi 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment