KOCHA CHARLES BONIFACE MKWASA AKIFUATILIA KWA UMAKINI MAZOEZI YA KIKOSI CHAKE |
Taifa Stars inashuka dimbani Jumapili kucheza mechi ya kirafiki
dhidi ya University of Pretoria maarufu kama Tucks FC.
Tucks inashiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini na mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya Stars inayotarajia
kuivaa Algeria Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa Stars, Charles Mkwasa amesema hiyo ni sehemu ya
kuanza kujipanga na kuangalia aina ya uchezaji.
“Umeona tokea tumeanza kambi mazoezi ni makali sana, taratibu
tunaanza kupunguza huku tukipata mechi hizo za kirafiki,” alisema Mkwasa
akizungumza na SALEHJEMBE jijini hapa.
Jumatatu iliyopita ndiyo Stars imetua Johannesburg kuanza
kambini hiyo iliyo katika hoteli ya kisasa yenye utulivu na ulinzi mkali ya Holiday
Inn Express.
Hoteli hiyo ipo katika eneo la Woodmead nje kidogo ya jiji la
Johannesburg na kuna utulivu mkubwa.
Imekuwa ikijifua katika viwanja vya St. Peters College pamoja na
kile cha Edenvale katika kitongoji cha Edenvale pia kipo nje kidogo ya jiji
hili kubwa nchini Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment