November 6, 2015


Kwa sasa uongozi wa Simba uko katika harakati za kutafuta wachezaji wapya kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo, Kocha wa Simba, Dylan Kerr, sasa amekubali.

Kocha huyo amekiri kuwa Simba ilifanya makosa kumuacha mshambuliaji Elias Maguli ambaye sasa anaitumikia Stand United.

“Nilifanya hivyo kwa sababu maalumu kwa ajili ya kuhakikisha tunasajili wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa zaidi yake lakini mambo yamekuwa tofauti.


“Maguli angeonyesha mapema uwezo wake kama alionao sasa, hakika nisingependekeza atolewe, lilikuwa ni kosa kumuacha,” alisema Kerr.

Tayari Maguri ameifungia Stand United mabao 9 huku Simba ikiwa ina mabao 15 ya kufunga katika kikosi chake chote. Upachikaji huo wa umemfanya Maguri arejee katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambacho sasa kimeweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria, Novemba 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic