Mechi kati ya Azam na Toto Africans ya Mwanza
uliopigwa wikiendi iliyopita uliweka rekodi ya aina yake baada ya kuwa pambano
lililopigwa kwa muda mrefu zaidi katika mechi zote za ligi mpaka sasa.
Pambano hilo lilimalizika kwa Azam inayonolewa na
Muingereza, Stewart Hall, kuibuka na ushindi wa mabao 5-0, rekodi hiyo ni mechi
kuchezwa kwa dakika 111 ikiwa ni zaidi ya dakika 21 za muda wa kawaida.
Kisa cha pambano hilo kupigwa kwa muda wote huo ni
kutokana na wachezaji wa Azam kupata madhara wakati mechi ikiwa inaendelea
ambapo wachezaji Jean Mugiraneza na kipa Aishi Manula waliomba udhuru wa kwenda
maliwatoni pamoja na kipa wa Toto, Mussa Mohammed, kutumia muda mrefu
akifanyiwa matibabu.
Kipindi cha kwanza cha pambano hilo baada ya kufika
dakika 45 za mapumziko mwamuzi wa mezani alionyoosha dakika tisa za nyongeza na
katika kipindi cha pili baada ya kufika dakika 45 mwamuzi huyo alinyoosha
dakika 12 za kuendelea mchezo huo akifidia muda ambao ulitumiwa na wachezaji
hao kwenda msalani.
Katika rekodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa siku za
hivi karibuni, hakuna mechi ambayo imechezwa kwa muda mrefu hivyo au wachezaji
wawili kwenda msalani wakati mchezo ukiendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment