November 8, 2015


Kama hukuwahi kusikia hili, acha nikueleze kuhusiana na ubabe wa Cristiano Ronaldo dhidi ya Sevilla.


Mreno huyo tayari amefunga hat trick tano katika mechi ambazo amekutana na kikosi hicho kigumu tokea alipotua Madrid akitokea Manchester United.

Pia amefunga jumla ya mabao 19 dhidi ya timu hiyo maarufu kama Andalusian. Alianza kuiadhibu katika mechi ya msimu wa 2010-11 alipofunga mabao manne katika ushindi wa 6-2.

Baada ya ushindi huo, Ronaldo aliendelea kufunga hat trick moja katika kila msimu dhidi ya timu hiyo, rekodi ambayo haijawahi kuwekwa na mchezaji yoyote yule tokea kuanza kwa La Liga.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic