Mshambuliaji nyota wa Taifa Stars,
Mbwana Samatta amewatoa hofu Watanzania kwa kuwaambia hana uchovu wowote na
atajituma kadiri ya uwezo wake kuipa ushindi Tanzania dhidi ya Algeria, leo
Jumamosi.
Samatta ataichezea Taifa Stars dhidi ya
Algeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mechi ya kufuzu Kombe la Dunia
2018 akiwa ametoka kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika klabu yake ya TP
Mazembe ya DR Congo.
Samatta alisema kuwa yupo fiti kwa
ajili ya mechi hiyo ya Algeria kutokana na maandalizi waliyoyafanya chini ya
Kocha Charles Mkwasa.
Pia Samatta alisema, juzi jioni alikaa
pamoja na wachezaji wenzake kwa ajili ya kuwapa morali na kuwatoa hofu ya
mchezo huo ili kuhakikisa wanashinda nyumbani kabla ya kwenda kurudiana
ugenini.
“Watanzania wengi wana hofu kuwa uhenda
nikawa nimechoka na nikashindwa kucheza mechi ya kesho (leo) dhidi ya Algeria,
kitu ambacho siyo sahihi.
“Ningependa kuchukua muda huu kuwatoa
Watanzania kuwa nipo fiti kwa ajili ya mechi na Algeria, licha ya kucheza
fainali wikiendi iliyopita ya michuano ya Afrika.
“Kikubwa nilichopanga mimi na wachezaji
wenzangu ni kuipa sifa nchi yangu kwa kuhakikisha tunawafunga Algeria na
kusonga mbele kwenye michuano hiyo,” alisema Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment