KAMBI YA TAIFA STARS JIJINI JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI |
Na Saleh Ally, Johannesburg
KAMBI ya Taifa Stars iko katika hoteli ya Holiday Inn jijini
hapa na ulinzi ni mkali hasa.
Mazingira ya kambi hiyo yako katika utulivu sana na uzio wote
umezungushiwa nguzo za umeme.
Anayeingia lazima anahojiwa na askari zaidi ya wanne ambao
wanakuwa kwenye lango kuu la kuingilia.
Hata akiingia analazimika kuyapita majengo matatu kabla ya
kufikia hoteli iliyo.
Hakuna sehemu yoyote ya karibu kwa ajili ya vinywaji au mtu
anaweza kwenda kutembelea, badala yake hata kama ni maji au mahitaji ya ziasa
ya wachezaji angalau takribani kilomita 2 yanaweza kupatikana.
Mratibu wa Taifa Stars, Msafiri Mgoyi amesema wamefanya hivyo
ili kuweza kufikia malengo.
“Hii ni timu ya taifa, suala la usalama ni la kwanza. Lakini
tunaangalia utulivu pia na kuhakikisha wachezaji wanapumzika,” alisema.
Stars inajiandaa kuivaa Algeria Novemba 14 jijini Dar es Salaam katika harakati zake za kuwania kucheza Kombe la Dunia. Mechi ya marudiano itachezwa Novemba 17 jijini Algers.
0 COMMENTS:
Post a Comment