Taifa Stars leo imemaliza programu yake ya mazoezi katika kambi ya hapa
jijini Johannesburg kujiandaa na mechi yake dhidi ya Algeria.
Mazoezi ya leo yamefanyika kwenye Uwanja wa Edenvale jijini hapa na
baada ya hapo, Stars kesho saa 10 jioni hapa na 11 nyumbani inashuka dimbani
kuwavaa timu ya taifa ya Afrika Kusini chini ya miaka 23.
Tayari Afrika Kusini imetangaza kikosi chake ambacho kitaivaa Stars hiyo
kesho.
Kwa mujibu wa Kocha Charles Boniface Mkwasa, wachezaji wa Stars
watapasha kidogo kuweka miili sawa kwa ajili ya mechi hiyo ya kesho.
0 COMMENTS:
Post a Comment