TP Mazembe wamechukua ubingwa wa Afrika baada ya
kuitwanga USM Alger ya Algeria kwa mabao 2-0.
Mashujaa wa Mazembe katika mechi ya leo walikuwa ni
Mtanzania, Mbwana Samatta aliyefunga bao
la kwanza kabla raia wa Ivory Coast, Roger Assale akifunga la pili akimalizia
kazi nzuri ya Samatta.
Samatta ndiye
alianza kufunga bao la kwanza katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa pelnalti likiwa
ni la pili kwake katika michezo miwili ya fainali kwa kuwa alifunga moja
waliposhinda 2-1 ugenini.
Bao hilo ni
la saba kwa Samatta, bao hilo linamfanya kujumuika na Bakry 'Al Medina' Babiker
raia wa Sudan anayekipiga Al Merrikh. Hao sasa ndiyo wanakuwa wafungaji bora.
Assale ndiye
alimaliza kabisa juhudi za Walgeria hao ambao walionekana kusaka angalau bao
moja la ugenini baada ya kufunga bao katika dakika za majeruhi kwa kuugusa tu
baada ya pasi saafi ya Samatta akiwa ameuwahi mpira mrefu na kuongoza counter
attack iliyomaliza kazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment