November 8, 2015

Watanzania wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu leo ni tegemeo la TP Mazembe katika mechi ngumu ya pili ya fainali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wachezaji dhidi ya USM Alger ya Algeria safari hii MAzembe wakiwa nyumbani Lubumbashi.

Jana kulikuwa na sala maalum mjini Lubumbashi na wachezaji, viongozi na mashabiki wa TP Mazembe walijumuika kanisani.

Mechi ya kwanza, TP Mazembe ikiwa ugenini ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na sasa inahitaji sare ya aina yoyote au kuibuka na ushindi tena.

Kila upande wa TP Mazembe unajua ugumu wa mechi hiyo. Hivyo wamejiandaa vilivyo na Samatta amesema watapambana hadi kieleweke.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic