Wachezaji wa Yanga
wamepewa mapumziko ya siku 10 kabla ya kurejea kazini.
Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm ameamua kutoa ofa hiyo kwa wachezaji wake kutokana na ligi kusimama.
Hata hivyo wachezaji
hao wametakiwa kurejea kazini Vovemba 12 kuanza kujifua.
Meneja wa Yanga,
Hafidhi Saleh amesema kikosi hicho kitaanza kujifua Novemba 12 isipokuwa
wachezaji walio katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kitakachocheza
Novemva 14 dhidi ya Algeria.
“Wale walio katika timu
ya taifa ya wanaocheza Novemba 14, pia watakaokwenda katika timu nyingine za
taifa.
“Tutaanza mazoezi
taratibu na baada ya wale walio katika vikosi vya taifa, wataungana na wenzao
na kuendelea na programu,” alisema Saleh.
Baada ya mechi 9, Yanga
ambao ni mabingwa watetezi wamebaki katika nafasi ya pili katika msimamo wa
Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 23 nyuma ya vinara Azam FC wenye 25.







0 COMMENTS:
Post a Comment