MAYANJA (KULIA) |
Huku kukiwa na
hali ya sintofahamu kwa timu ya Coastal Union kama ni kumtosa au kuendelea na
Mganda, Jackson Mayanja kuinoa timu hiyo, ghafla Kiyovu Sports ya Rwanda
imeibuka na kutaka huduma ya kocha huyo.
Mayanja ambaye
amekosa matokeo mazuri kwenye mechi za awali za Coastal, amekuwa akihusishwa
kuvunjiwa mkataba na timu hiyo lakini uongozi umekuwa ukikosa jibu la moja kwa
moja kuhusiana na ishu hiyo.
Mmoja ya marafiki
wa karibu na kocha huyo aliyepo Uganda kwa sasa akimuuguza mama yake,
amesema kuwa Kiyovu wamempigia simu na kumueleza dhamira
yao lakini bado hawajakubaliana moja kwa moja.
“Zipo timu mbili
zinamtaka, lakini Kiyovu ndiyo wamempigia simu, yeye (Mayanja) amewaambia
kwamba wasubiri kwanza amalize kumuuguza mama yake ambaye amefanyiwa upasuaji
wa tumbo hivi karibuni, baada ya hapo watazungumza, maana anaheshimu mkataba wa
Coastal pia,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa
Mayanja kuzungumzia suala hilo, alisema kwa kifupi: “Nani amekwambia? Ni kweli Kiyovu
nimewasiliana nao lakini hatujafikia popote, maana bado nipo ndani ya mkataba
na Coastal kwa sasa.”
0 COMMENTS:
Post a Comment