December 22, 2015


Uongozi wa Yanga umesema umeshatuma majina ya wachezaji watakaoitumikia klabu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jina pekee ambalo halijatumwa ni la mshambuliaji Paul Nonga ambaye amejiunga na timu hiyo wiku nne zilizopita akitokea Mwadui FC.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema kila kitu kimekamilika.

“Tayari tumeshatuma majina na kila kitu kimekamilika. Ndiyo maana ninawashangaa TFF kusema tunatakiwa kukamilisha zoezi hilo,” alisema Muro.


Awali TFF ilikuwa imezitaka Yanga na Azam FC kuhakikisha zinatuma majina na kukamilisha taratibu zote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic