Nyota wakubwa duniani katika soka kama David Beckham, Louis Figo, Alexandro del Piero, Robert Pires, Deco; Dwight Yorke; Andriy Shevchenko na Roberto Carlos waliungana tena na kucheza mechi pamoja nchini Kuwait.
Ilikuwa mechi maalum kufungua Uwanja wa Jaber Al-Ahmad unaobeba watazamaji 60,000 na watandelea na ziara hiyo katika nchi za Kiarabu.
Pamoja na Figo na Pires kutupia, lakini mechi hiyo iliisha kwa wakali hao kulala kwa mabao 4-2 dhidi ya nyota wa Kuwait wanaocheza katika timu mbalimbali za Ligi Kuu.
KIKOSI CHAO KILIVYOKUWA:
(4-4-2):
Jens Lehmann; Gianluca Zambrotta, Michel Salgado, Alessandro Nesta, Roberto Carlos; David Beckham, Luis Figo, Robert Pires, Deco; Dwight Yorke; Andriy Shevchenko.
Subs: David James, Carles Puyol, Mohamed Aboutrika, Del Piero
Manager: Fabio Capello
DAIL MAIL




















0 COMMENTS:
Post a Comment