December 24, 2015


Ile taarifa ya mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Samatta kusajiliwa na  KRC Genk ya Ubelgiji.

Taarifa hiyo ya kumalizana kwake imepatikana leo mchana ingawa meneja wake, Jamal Kisongo ameendelea kusisitiza mambo hayajaisha vizuri.

Taarifa zinaeleza kuwa Samatta ameisharejea nchini kwa ajili ya mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya DR Congo.

Timu inayoelezwa kumsajili Samatta itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Awali ilielezwa mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi alitaka dau la zaidi ya euro milioni mbili, jambo ambalo lilionekana kuwashinda Genk.

Hata hivyo waliomba kujipanga na leo ukafanyika mkutano baina ya pande hizo mbili kumalizana.

"Bado mkutano unaendelea, kama mambo yatakuwa poa nitawaeleza," alisema Kisongo.

Alipopigiwa Samatta, yeye aliahidi kupiga baadaye. "Nitakupigia baadaye kidogo." Hata hivyo baadaye hakupatikana.

Genk inatumia uwnaja wa Cristal Arena, imetwaa mataji matatu ya ligi kuu Ubelgiji mwaka
1998–99 ,2001–02 na 2010–11. 

Klabu hiyo pia imekusanya nafasi za kucheza Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi katika miaka hii ya 
2008–09 na 2012–13.

Kama Genk imemalizana na Mazembe na Samatta, utakuwa ni wakati mwingine kama hatua ya soka la Tanzania kama changamoto kwa vijana.

Samatta amekuwa na mafanikio makubwa akiwa na kikosi cha Mazembe.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic