December 16, 2015

MAJIMAJI

Kama unakumbuka, msimu uliopita mpaka ligi inamalizika, Coastal Union ilikuwa na rekodi ya timu ambayo ilifungwa mabao mengi katika mchezo mmoja baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Yanga cha mabao 8-0, lakini safari hii Majimaji nayo imeanza hivyo.

Ingawa ligi bado mbichi, imecheza michezo 11 pekee na kushinda michezo mitatu tu chini ya Kocha Mika Lonnstrom raia wa Finland na kuweza kuandika rekodi yake kwa kuwa ndiyo timu ambayo imepokea vipigo vya nguvu kwenye ligi.

Majimaji imeambulia vipigo vizito kutoka kwa Simba katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa ambapo walipigwa mabao 6-1 na mchezo mwingine ni ule dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba waliopanda nao daraja. Walichapwa mabao 5-1.

Timu hiyo ambayo inashika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu ikiwa imeshinda michezo mitatu na kutoa sare mbili huku ikipoteza michezo sita, mpaka sasa ina jumla ya pointi 11.


 Vipigo vingine vikubwa kwenye ligi hiyo tofauti na Majimaji ni pamoja na ule mchezo wa Azam dhidi ya Toto Africans, ambapo Azam walitoa dozi ya mabao 5-0, JKT Ruvu 4-0 Tanzania Prisons, JKT Ruvu 2- 4 Azam, Mtibwa Sugar 4-1 Mwadui FC, Yanga 4-1 Toto Africans na  Yanga 4-1 JKT Ruvu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic