Tena kwa kushitukiza, hali ya hatari imetangazwa kwa timu yoyote
itakayokutana na JKT Ruvu inayonolewa na Kocha Abdallah Kibadeni katika mechi
za Ligi Kuu Bara kuwa ni lazima ifungwe.
Kibadeni ametoa kauli hiyo huku kesho Jumapili
timu yake ikicheza na Coastal Union kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam
katika muendelezo wa ligi kuu.
Alisema; “Ninachoangalia sasa katika ligi ni
kushinda kila mechi bila ya kujali tunakutana na timu yenye kiwango kipi, sisi
hatujali hapa yeyote anayekuja mbele yetu tutahakikisha tunamfunga.
“Ushindi tulioupata wikiendi iliyopita dhidi ya
Prisons (mabao 4-0) ni ishara kuwa kikosi kinaonyesha mwanga wa mafanikio,”
alisema. JKT Ruvu na Coastal Union zote zina pointi nane lakini Coastal ipo juu
katika nafasi ya 13 kwani ina tofauti kubwa ya mabao kuliko JKT iliyo nafasi ya
14.







0 COMMENTS:
Post a Comment